Mwekezaji wa klabu ya Simba Mohammed Dewji 'Mo' ameibua wazo la kununua timu ya daraja la kwanza ambayo itakuwa timu ya pili ya Simba
Akizungumza kwenye hafla ya uwekaji jiwe la msingi uwanja wa Simba ulioko Bunju leo, Mo alisema timu hiyo itasajili kikosi cha vijana cha Simba na itatumika kuandaa wachezaji ambao watasajiliwa na timu ya wakubwa na wengine kuuzwa kwenda timu nyingine
Mo amesema timu hiyo itaitwa Simba Sc na itakuwa ikishiriki ligi daraja la kwanza na madaraja ya chini tu hata ikitokea imepanda ligi kuu itabaki hukohuko

No comments:
Post a Comment