Amewataka vijana kuachana na tabia ya kukatishana tamaa, kuwataka kutumia muda kufurahia matokeo ya kazi inayofanywa na Serikali kuanzia mwaka 2015.
Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Agosti 28, 2019 katika Shule ya Msingi Ubungo Kisiwani wilayani Ubungo katika siku ya pili ya ziara yake jijini Dar es Salaam.
"Muda wa kupata mapato ya dezo umepita, uvivu ni adui wa maendeleo, tusikatishe tamaa tunaposherehekea matokeo ya kazi yetu kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM,” amesema.
Huku akishangiliwa na mamia ya watu waliojitokeza kumsikiliza, Dk Bashiru amesema kama vyuma vimekaza kwa sababu ya kuokoa maisha ya watoto, waache vikaze.
"Kama tunakazwa na vyuma kwa sababu ya kujenga shule, kuokoa vifo vya akina mama na watoto, kulinda uhuru, amani yetu basi vyuma hivyo vitukaze mpaka tushike adabu."
"Lakini najua wanaosema vyuma vimekaza ni waliozoea kupiga dili, huwezi kufanya kazi ya neema, kheri halafu ukatafuta mchawi," amesema.

No comments:
Post a Comment