Yanga imeanza kwa kuchechemea ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2019/20 baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Ruvu Shooting
Ruvu Shooting walijipatia bao lao kwenye dakika ya 20 kipindi cha kwanza
Licha ya kutawala mchezo huo kwa muda mwingi, safu ya ushambuliaji Yanga ilishindwa kumaliza nafasi nyingi walizotengeneza
Bado kocha Mwinyi Zahera ana kazi ya kutengeneza muunganiko wa safu hiyo kwani haiko sawa
Ruvu Shooting imepata ushindi kwa mara ya kwanza baada ya timu hizo kukutana mara 13 Yanga ikiibuka kidedea mara zote

No comments:
Post a Comment