We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Sunday, August 4, 2019

Dk Bashiru afafanua misingi mikuu mitatu ya Chama cha Mapinduzi


Katibu Mkuu wa CCM,  Dk Bashiru Ally ameelezea misingi mikuu mitatu ya chama hicho na kuwataka viongozi wa mashina kuifuata.

Akizungumzia jana Jumamosi Agosti 3, 2019 wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuimarisha demokrasia katika mashina ya CCM.
Alitaja misingi hiyo kuwa ni pamoja na kuhakikisha kila kikao ama shughuli yoyote iwe na balozi,  viongozi wa mabaraza ya wazee na vikundi vya ngoma.
Dk Bashiru ambaye pia ni mlezi wa CCM Mkoa wa Mwanza, amesema wilaya yoyote atakayotembelea na kukuta watu wa namna hiyo, atasusia kikao au atawapunja kwenye hotuba.
Katibu huyo pia ameagiza  balozi yeyote hatakiwi kupanga foleni kwenye ofisi za umma.
Amesema viongozi hawa ndiyo walifanya jitihada za kuhakikisha chama cha Tanu na CCM  vishinde  na ndiyo wanajua siri zao zote  na kwamba, wanafanya kazi usiku na mchana na kwa kujitolea.
Kuhusu kuwepo kwa mabaraza ya wazee, ameagiza ifikapo Septemba 30, mwaka huu  kila shina nchini kote lihakikishe linapeleka ripoti ya kuundwa kwa mabaraza hayo.
Katika hatua nyingine,  Dk Bashiru amewataka viongozi wa CCM kufanya vikao vyenye maslahi na chama chao na kama ni vya kumpitisha mtu wafanye hivyo na si kuwakatilia mbali.
Akizungumzia kuwapo kwa malalamiko ya wanachama wanaohamia kwenye chama hicho kutoka vyama vingine, amesema wasibaguliwe kwa kuwa wana haki na wajibu sawa na wengine

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list