Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo itashuka dimba la Kasarani nchini Kenya kuumana na Harambee Stars katika mchezo wa kusaka nafasi ya kutinga fainali za CHAN 2020 kwa wachezaji wa ndani
Stars itakuwa na kazi ya kufanya leo ugenini kwani itahitaji kuibuka na ushindi ili iweze kusonga mbele
Katika mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Taifa wiki iliyopita, timu hizo zilitoka suluhu ya bila kufungana
Kaimu Kocha Mkuu wa Stars Etienne Ndayiragije amesema wamefanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza kwenye mchezo wa kwanza
Hivyo wana matumaini makubwa ya kushinda mchezo wa leo
Mchezo utapigwa kuanzia saa kumi jioni

No comments:
Post a Comment