Mchezo wa kirafiki kati ya Yanga dhidi ya Friends Rangers uliopigwa asubuhi ya leo Jumanne, Julai 30 umemalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0
Mabao ya Yanga kwenye mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Chuo cha Biblia, Bigwa mkoani Morogoro yalifungwa na Sadney Urikhob kwenye dakika ya 38 na bao la pili kufungwa na Papi Tshishimbi kwenye dakika ya 68
Huo ulikuwa mchezo wa sita wa kukipima kikosi cha Yanga, ambapo mabingwa hao wa kihistoria wameshinda michezo yote
Katika michezo hiyo, ukuta wa Yanga umeruhusu kufungwa bao moja tu huku wakifanikiwa kufunga mabao 25
Mchezo huo pia umempa nafasi kocha Mwinyi Zahera kuwapima wachezaji wake, ukiwa ni mchezo wa pili kuushuhudia tangu aliporejea nchini
No comments:
Post a Comment