Kwa mara ya kwanza Cristiano Ronaldo amekutana na Rais wa klabu yake ya zamani Real Madrid, Florentino Perez tangu alipoachana na timu hiyo na kujiunga na kibibi kizee cha Turin.
Ronaldo amekutana na Perez wakati mchezaji huyo akikabidhiwa tuzo ya Marca’s Legend award usiku wa jana siku Jumatatu.
Imewahi kuripotiwa mara kadhaa kuwa wawili hao hawana mahusiano mazuri na kabla ya kuondoka Madrid, huku ikiaminika kuwa Perez ndiyo sababu kubwa ya mshambuliaji huyo kutimka.
Marca imekuwa na kawaida ya kutoa tuzo kwa mwanamichezo mmoja mmoja tangu kuanzishwa kwake mwaka 1997. Mara baada ya kukutana wawili hao ghafla baadhi ya mashabiki nchini Hispania wametaka staa huyo arudishwe Madrid.
Ronaldo anaungana na mastaa wengine kama Michael Jordan, Pele, Rafa Nadal, Novak Djokovic, Muhammad Ali, Usian Bolt, Michael Phelps, Michael Schumacher and Diego Maradona katika kuchukua tuzo hiyo. Hasimu wa Ronaldo ambaye ni mchezaji wa Barcelona, Lionel Messi amewahi kuchukua tuzo hiyo mwaka 2009.
Kwa upande wake Ronaldo amesema kuwa kupata kwa tuzo hiyo ni matokeo ya mafanikio makubwa aliyopata wakati akiwa katika miamba hiyo ya soka Hispania Real Madrid.
No comments:
Post a Comment