Akifungua kongamano la Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi linalofanyika mjini Shinyanga jana Julai 3, 2019, Mhagama ametaja fursa zinazoambatana na mradi huo unaopita kwenye mikoa minane kuwa ni pamoja na ajira, biashara na huduma mbalimbali za chakula, malazi na makazi kwa watumishi.
“Watanzania watakaopata fursa ya ajira katika mradi huu, watumia nafasi hiyo kujifunza na kupata ujuzi na teknolojia mpya kutoka kwa wageni watakaoajiriwa katika mradi huu,” amesema Mhagama.
Katibu mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi, Beng’I Issa ametaja sekta ya ujenzi, afya, kilimo (chakula), mawasiliano na huduma za kijamii kuwa miongoni mwa maeneo muhimu yatakayonufaika.
“Asilimia 60 ya kazi ya ujenzi wa bomba hilo la mafuta itafanyika upande wa Tanzania huku asilimia 40 inayosalia, ndiyo itahusu upande wa Uganda. Tuchangamkie fursa hiyo,” amesema Issa.
Kwa upande wa Tanzania, mradi huo unapita kwenye mikoa minane, wilaya 24 na vijiji 134 ambako nafasi za ajira ya muda zaidi ya 10,000 na nyingine 1,000 za kudumu zinatarajiwa kupatikana maeneo hayo huku moja kati ya vituo vinne vya ujenzi kinatarajiwa kujengwa wilaya ya Nzega mkoani Tabora.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack amewataka wakazi mkoani humo kujipanga kutumia kila aina ya fursa itakayojitokeza huku Mwenyekiti wa Bodi ya Haki Rasilimali, Dolnad Kasongi akiahidi kuwa bodi hiyo itatoa elimu kwa wananchi katika maeneo bomba hilo linakopita ili waweza kutumia fursa za kiuchumi zitakazojitokeza.

No comments:
Post a Comment