Baadhi ya vyombo vya habari nchini Afrika Kusini vimeripoti kuwa mshambuliaji Emmanuel Okwi anakaribia kusajiliwa na Kaizer Chiefs ya nchini humo
Kaizer Chiefs tayari imemsajili aliyekuwa kiungo wa Simba James Kotei kwa mkataba wa miaka mitatu
Okwi amehusishwa na timu hiyo tangu wakati wa usajili wa dirisha dogo
Hata hivyo Mganda huyo bado yuko kwenye mazungumzo na uongozi wa Simba mvutano ukibaki kwenye suala la mkataba
Wakati Simba ikimtaka asaini mkataba wa miaka miwili, yeye anataka mwaka mmoja ambao inaelezwa utaigharimu Simba Milioni 115
Simba imebaki na nafasi mbili za wachezaji wa kigeni na inaelezwa nafasi moja itachukuliwa na beki Zana Coulibaly ambaye tayari yuko nchini
Nafasi nyingine itachukuliwa na kiungo Francis Kahata ambaye taarifa za awali zimebainisha kuwa tayari amesaini mkataba wa miaka mitatu nchini Misri

No comments:
Post a Comment