We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Thursday, July 4, 2019

ZAHERA AWAKA KUHUSU GADIEL MICHAEL “MNAMBEMBELEZA WA NINI?”

KOCHA Mkuu wa Yanga Mkongomani, Mwinyi Zahera amesikia taarifa za beki wake wa pembeni, Gadiel Michael kugomea kusaini mkataba akasonya na kuwaambia viongozi; “Mnambembeleza wa nini?”

Hiyo, ikiwa ni siku chache tangu mmoja wa viongozi wa Yanga kusafiri na mkataba hadi nchini Misri inapofanyika Afcon kwa ajili ya kumsajili beki huyo aliyekuwa Taifa Stars iliyoondolewa katika michuano hiyo.

Beki huyo kwa mara ya pili amegomea kusaini mkataba baada ya hivi karibuni kukataa dau la Shilingi Milioni 50 alilowekewa mezani huku Simba ikielezwa kumuwekea 70 ambazo ameshawishika kusaini miaka mitatu Msimbazi.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, Zahera tayari amewaambia mabosi wa timu hiyo kuachana na mchezaji huyo kwavile si staa kiasi hicho wala gharama yake si kubwa kiivyo.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, kocha huyo tayari ametoa mapendekezo ya kumbakisha Haji Mwinyi aliyekuwa kwenye mipango ya kuachwa kwa ajili ya kusaidiana na Ally Mtoni ‘Sonso’.

Aliongeza kuwa, kocha anaamini kuwa wapo wachezaji wengine wenye uwezo mkubwa zaidi ya Gadiel, hivyo kuondoka kwake hakutamuumiza huku akimtakia kila heri huko aendako.

Habari zinasema Mwenyekiti wa timu hiyo, Mshindo Msolla ametoa mpaka kufikia leo Gadier kuelezea hatma yake kusaini Yanga kabla ya wao uongozi kufanya uamuzi.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list