Wakazi wa kata ya Kijombe wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe wamelalamikia kukosekana kwa dawa katika kituo cha afya Wanging'ombe na kwenye zahanati ya kijiji chao.
“Tunategemea kuwa Kijombe ndio mkombozi wetu lakina sasa pale dawa hamna,mfano mimi kuna siku nilipeleka mgonjwa wangu mjamzito alipasuliwa na nilitumia laki moja na elfu tatu mia tano,kwa tunaona yamejengwa majengo lakini madawa hayupo mle ndani”walisema baadhi ya wananchi
Diwani wa kata ya Kijombe Nashon Kilamlya amesema wakazi wake wamekuwa wakikosa dawa pindi wanapofika katika zahanati ya Kijombe na kwenye kituo cha afya huku akielezwa zipo pindi anapofuatilia
“Sisi tunapouliza kwenye vikao tunaambiwa dawa zipo lakini wagonjwa wanapoenda unakuta dawa fulani hazipo waende wakanunue madukani,na hilo ndio tatizo na mala nyingi tunafuatilia kujiridhisha lakini majibu ndio hayo”alisema Nashon Kilamlya
Mbunge wa jimbo la Wanging'ombe mhandisi Gerson lwenge amekiri kupokea malalamiko hayo na kwamba atakwenda kufuatilia kuona tatizo hilo likoje ilihali serikali ilitangaza kuwapo kwa dawa za kutosha.
“Sasa mimi nashangaa kusikia hakuna dawa kwasababu serikali imetoa fedha nyingi sana kwa ajili ya ununuaji wa madawa na vifaa tiba,naomba hili nilifuatilie ili nione kilichotokea, labda inawezekana wakati huo aina ya dawa anayohitaji mgonjwa haipatikani kulingana na matatizo aliyo kuwa nayo kwasababu kuna baadhi ya dawa huwa haziwekwi kwenye vituo vya afya”alisema Lwenge
Tatizo la upatikanaji wa dawa kwa wakazi mbalimbali nchini lilielezwa kukoma kutokana na kutengwa kwa bajeti ya zaidi ya shilingi bilioni 270 katika mwaka wa fedha uliopita kwa ajili ya ununuzi wa dawa lakini bado tatizo hilo lingali kwa baadhi ya sehemu za kutolea huduma ya afya.



No comments:
Post a Comment