We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Monday, July 8, 2019

Dk Bashiru awaonya wanasiasa waropokaji

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ally amewaonya wanasiasa nchini Tanzania kuachana na tabia ya kuropoka maneno yanayoweza kuhatarisha usalama wa Taifa.
Ametoa kauli hiyo jana Jumapili Julai 7, 2019 katika kikao cha ndani kilichofanyika Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro na kuwahusisha viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama hicho tawala nchini Tanzania.
Dk Bashiru aliyepo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku nne amesema wanasiasa wakianza kuropoka nchi itapotea.
“Mtu akiropoka mnamjibu palepale ili kutuliza hali ya hewa kwa sababu waropokaji hawapo Kenya peke yake na Tanzania wapo,” amesema Dk Bashiru akitolea mfano kauli isiyofaa iliyotolewa hivi karibuni na mwanasiasa mmoja nchini Kenya.
Alitumia nafasi hiyo kuwataka viongozi wa chama na Serikali kuwa makini na taarifa za upotoshaji, kutoamini kila taarifa wanayoiona mitandaoni.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list