Kiungo Papi Tshishimbi ameteuliwa kuwa nahodha wa kikosi cha Yanga, akichukua majukumu hayo kutoka kwa Ibrahim Ajib aliyetimkia Simba
Kwenye majukumu yake hayo mapya, Tshishimbi atashirikiana na mkongwe Mrisho Ngasa ambaye taarifa zimebainisha kuwa ameteuliwa kuwa nahodha msaidizi
Mkongwe Kelvin Yondani alikuwa nafasi kubwa ya kurudishiwa kitambaa cha unahodha, hata hivyo kitendo cha kutoripoti kambini mkoani Morogoro kimemuondolea sifa
Aidha hatma ya Juma Abdul aliyekuwa nahodha msaidizi, inasubiri maamuzi ya kocha Mwinyi Zahera
Abdul na Andrew Vicent nao hawakuripoti kambini Morogoro na wanasubiri uamuzi wa Zahera
Wawili hao wako hatarini kutemwa kwani wamekosa program za mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya
Tshishimbi na Ngasa ni wachezaji mfano kwa wengine kwani wanaipigania Yanga kwelikweli, iwe mazoezini au kwenye mechi
No comments:
Post a Comment