Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola, amesema mpango wa Serikali ni kuhakikisha inatokomeza biashara haramu ya usafirishwaji wa binadamu unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara kwa nia ya kujipatia kipato.
Waziri Lugola ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam, wakati wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya kudhitbiti biashara ya binadamu, ambapo amesema biashara hiyo kwa sasa ni sawa na biashara ya utumwa.
"Biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu hapa nchini inayoongoza ni ya kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine waathirika ni watoto wadogo, wasichana na vijana ambao wako katika umri 13 hadi 24", amesema Kangi Lugola.
"Hali hii inaashiria kwamba kuna utumwa, licha ya utumwa ambao tulifanyiwa na wenzetu wakati ule, bado wapo baadhi yetu wanaowafanya Watanzania wenzetu kuwa watumwa", amesema Kangi Lugola.
Siku ya kupinga biashara ya binadamu kimataifa huadhimishwa kila Julai 30, ya kila mwaka.
No comments:
Post a Comment