Jukumu la kudhibiti chakula na vipodozi limehamishwa kutoka iliyokuwa mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), kwenda shirika la viwango Tanzania (TBS).
Hatua hii inakuja kufuatia mabadiliko ya sheria ya chakula, Dawa na Vipodozi sura ya 219 yaliyofanyika kupitia sheria ya fedha ya mwaka 2019.
Kufuatia mabadiliko hayo iliyokuwa TFDA kwa sasa, inatambulika kama Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ikiwa na jukumu la kudhibiti dawa, tiba na vitendanishi nchini.
Aidha TMDA imeainisha baadhi ya majukumu ambayo yatakuwa yakitolewa na TBS, ikiwa ni pamoja na kupokea maombi na usajili wa bidhaa zote za chakula na vipodozi zinazotengenezwa hapa nchini, au vile vinavyoingizwa kutoka nje ya nchi.
Majukumu mengine ni kufanya ukaguzi wa maeneo yote yanayojihusisha na utengenezaji, utunzaji, usambazaji na uuzaji wa chakula na vipodozi.
Mbali na hayo pia itatoa vibali vya uingizaji nchini na usafirishaji nje ya nchi, kwa bidhaa zote za chakula na vipodozi ikiwa ni pamoja na ukaguzi kwenye vituo vya forodha.
No comments:
Post a Comment