Nyota wa klabu ya Manchester City, Raheem Sterling amefunguka mazito kuhusu maisha aliyopitia wakati alipokuwa na umri mdogo, kuhusiana na kifo cha baba yake mzazi, kuchapwa na mkanda shuleni alipokuwa Jamaica na namna kocha wake Pep Guardiola alivyomtia moyo ndani ya timu hiyo ya Uingereza.
Mshambuliaji huyo wa mabingwa wa ligi kuu soka nchini Uingereza, Sterling ameyasema hayo wakati ambapo picha zake zinatarajiwa kutumiwa katika ukurasa wa mbele jarida la August’s edition of GQ magazine litakaloanza kupatikana siku ya Ijumaa.
Kwenye jarida hilo, Sterling ataonekana akiwa na mabawa mgongoni huku akiwa amevalia suruali nyeusi. Kwenye mahojiano hayo staa huyo alikuwa karibu kabisa na baadhi ya wachezaji wa timu yake.
Mbali na picha hizo kumuonyesha Sterling mwenye umri wa miaka 24 akiwa na mbawa kubwa za rangi nyeusi mgongoni na kuvalia ‘combat’ nyeusi, ‘bracelet’, saa lakini pia ameonekana akiwa cheni kubwa inayozunguka maeneo ya shingo yake wakati akiwa tumbo wazi.
Sterling ameishi Jamaica huku akiwa bila ya baba baada ya kuuawa wakati akiwa na umri wa miaka miwili pekee kisha miaka mitatu baadae ndipo akahamia jijini London.
Baba mzazi wa Raheem Sterling, Phillip Slater picha ikiwa imepigwa mwaka 1996 alipokuwa na miaka 29
Ameliambia jarida la GQ kuwa wakati mwingine ni vigumu lakini kila kitu hutokea kwa sababu maalumu, “Wakati mwingine ni vigumu lakini kila kitu hutokea kwa sababu.”
“Kwa sasa nina wangu, nitahakikisha nawapatia mapenzi kutoka kwa baba yao ambayo mimi mwenye sikuwahi kuyapata. Na nafikiri nitajiskia furaha hata na mimi mwenyewe.” – Amesema Sterling.
“Kwa maa ya kwanza iliniwia ugumu, kama unavyofahamu shule ni kitu cha tofauti. Hapa kuna shule nyingi lakini wakati nilipokuwa Jamaica ni tofauti na uvumilivu ni sifuri.”
“Nafikiri Serikali ya kule ndiyo iliyokuwa ikichangia, kunawakati ukatili ulikuwa umezidi mashuleni.” Sterling na mpenzi wake, Paige Milian wamekuwa katika mahusiano kwa muda mrefu na kujaaliwa kuwa na watoto wawili ambao ni Thiago, two, na Melody Rose, seven.
Sterling akiwa na familia yake, mpenzi wake Paige Milian na watoto wao Thiago, two, na Melody Rose, seven
Sterling amekuwa katika kipindi kizuri sana kwenye nafasi yake ya ushambuliaji na kuisaidia klabu ya Manchester City kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza akiwa chini ya kocha Pep Guardiola.
Akimzungumzi kocha huyo, Sterling amesema amekuwa na mahusiano mazuri naye “Mara kadhaa amekuwa akinipatia changamoto, amekuwa haniachi hata ni pumzike, kila mwaka amekuwa akisajili mchezaji ambaye anacheza nafasi yangu.”
No comments:
Post a Comment