Simba imemtambulisha mshambuliaji mpya Deo Kanda (29) aliyetua kwa mkopo kutoka klabu ya TP Mazembe, mabingwa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Kanda amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuwatumikia mabingwa hao wa Tanzania Bara
Taarifa iliyotolewa na uongozi wa Simba leo saa saba, imethibitisha kusajiliwa kwa nyota huyo
"Kazi ya kusajili wakali watakaohakikisha kikosi cha Mabingwa kinazidi kuwa tishio kwa wapinzani inaendelea"
"Mshambuliaji raia wa Congo DR, Deo Kanda (29) amejiunga na Mabingwa wa nchi.
"Kanda amesaini mkataba wa mwaka mmoja kukipiga Msimbazi akitokea TP Mazembe ambapo alikuwa mmoja wa wachezaji ambao waliiwezesha kushinda Ubingwa wa Afrika mwaka 2009, 2010 (aliifungia goli kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Esperance) na 2013 lakini pia akiwa ameshiriki Kombe la Dunia la Vilabu mwaka 2009, 2010, 2013"
Usajili wa Kanda kutua Simba ulifichuliwa mapema wiki hii na klabu ya TP Mazembe kupitia ukurasa wake rasmi wa mtandao wa Instagram
No comments:
Post a Comment