Aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ameshangazwa na hatua ya Spika Ndugai kutangaza kuwa jimbo lake liko wazi kwa kutohudhuria vikao vya Bunge, huku akieleza Spika anafahamu alipo kwa sababu alishawahi kutembelewa na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson akiwa nchini Ubelgiji kikazi.
Tundu Lissu ametoa kauli hiyo akiwa nchini Ubelgiji wakati akizungumzia juu ya maamuzi ya Bunge kutangaza kuwa jimbo lake liko wazi, kutokana na Mbunge huyo kutohudhuria vikao vya Bunge kwa muda mrefu.
Akizungumza kutokea nchini Ubegiji Tundu Lissu amesema kuwa "maafisa wa Ubalozi wa Tanzania hapa Ubelgiji waliniomba kukutana na wageni wa Kibunge na Kiserikali waliokuja kikazi Ubelgiji mfano Machi 2018 walinijulisha juu ya ujio wa Naibu Spika Tulia Ackson aliyetaka kuonana na mimi."
"Ni kweli sijawahi kuhudhuria kikao cha Bunge tangu Septemba 07, 2017 wala kuandika barua ya Kibunge kuhusu afya yangu kwa sababu Spika Ndugai alikuwa anajua kuhusu afya yangu." amesema Lissu
"Rais Magufuli anajua mimi nilipo ndiyo maana alimtuma Makamu wa Rais kuja kuniona Nairobi, Spika Ndugai anafahamu mimi nilipo hata kama hajawahi kuja kuniona licha ya kuahidi hadharani, yeye anafahamu nilipo kwa sababu Katibu wa Bunge anajua nilipo." ameongeza Mbunge Lissu
Julai 28 akiwa jijini Dodoma Spika wa Bunge Job Ndugai alitangaza kuwa jimbo la Singida Mashariki liko wazi, kutokana na Tundu Lissu kutohudhuria vikao vya Bunge.
No comments:
Post a Comment