Hakuna tena wasiwasi baada ya winga teleza Mrisho Ngasa kuthibitisha kuwa ameongeza mkataba kuendelea kukipiga Jangwani
Ngasa alikuwa aliwaniwa na timu kadhaa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Lakini leo amethibitisha, haelekei huko baada ya kuongeza mkataba Yanga
Ukizungumzia wachezaji waliofanya vizuri kwenye kikosi cha Yanga msimu uliopita, Ngasa ni mmoja wao
Hakuna shaka msimu ujao unaweza kuwa mzuri zaidi kwa mwamba huyo kutoka Kanda ya Ziwa kwani atacheza kwenye kikosi kilichosheheni mafundi wengi wa mpira

No comments:
Post a Comment