Mo Ibrahim alijiunga na Simba akitokea Mtibwa Sugar hakuwa na msimu mzuri katika klabu hiyo kutokana na kukosa nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza chini ya kocha Patrick Aussems.
Kwa mujibu wa chanzo cha ndani kutoka Simba kimedai kutokana na kushindwa kuwa na namba ya kudumu wameamua kumtoa kwa mkopo ili akakuze kiwango chake.
"Mo ataenda Namungo kwa mkopo na tayari mazungumzo kati ya pande zote mbili Simba na viongozi wa klabu hiyo yamekamilika kinachosubiliwa ni muda tu na nyota huyo kuondoka kwenda kuanza mazoezi kwaajili ya msimu mpya wa ligi."
"Bado tunamkataba naye wa mwaka mmoja ambao ndio anaenda kuumalizia huko Namungo, lakini kama kiwango chake kitaonekana kuimarika anaweza kurudishwa na kama atashindwa kumshawishi tena mwalimu basi atatafuta timu nyingine ambayo ataona sawa kuichezea," alisema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Simba, Crescentius Magori alisema kocha ndiye atakayekuja kutoa ripoti ya mchezaji gani anatakiwa kubaki na nani anatakiwa kutolewa kwa mkopo.
"Hiyo taarifa hakuna mtu anayeweza kuzungumzia zaidi ya benchi la ufundi sijajua kama linaukweli kiasi gani tunaomba muda hadi kocha atakaporudi ili aweze kuzungumzia hilo," alisema Magori.

No comments:
Post a Comment