We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, July 9, 2019

Msaidizi wa Membe apatikana, mambo matano aliyozungumza

Leo July 9, 2019 Msaidizi wa aliekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Membe, Allan Kiluvya amepatikana baada ya kuwepo taarifa kuwa alikuwa ametekwa na watu wasiojulikana.
Nakusogezea mambo matano aliyozungumza Allan Kiluvya na waandishi wa habari baada ya kupatikana.
“Ni kweli mimi ni Msaidizi wa Membe na kuhusu watekaji walikuwa wanataka nini kwa kweli hilo siwezi kusema kwa kuwa tayari nimetoa maelezo Polisi na wao ndiyo watatoa hizo taarifa” Allan Kiluvya
“Walivyoniachia waliniuliza sehemu ipi itakuwa salama kwangu, nikawauliza kwanza hapa nilipo wapi wakaniambia ni Gongolamboto, nikawaeleza mimi nakaa Tabata Kinyerezi niacheni sehemu nitakayoweza kufika salama nyumbani” Msaidizi wa Membe, Allan Kiluvya
“Nimeshatoa maelezo yangu kituo cha Polisi Kawe na wao wataeleza ukweli wote wa tukio na wasiposema, kwa kuwa mimi ni mpenda ukweli nitaeleza ukweli wote” Msaidizi wa Membe, Allan Kiluvya
“Naamini Polisi watatoa ripoti kwa kile nilichoandika, naamini hawatotoka nje ya kile” Msaidizi wa Membe, Allan Kiluvya
“Naamini nitaendelea kuwa Msaidizi wa Membe” Msaidizi wa Membe, Allan Kiluvya

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list