Yanga itaanza kampeni ya ligi kuu msimu huu baada ya kumaliza michezo ya hatua ya awali michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Mchezo wa kwanza itacheza dhidi ya Ruvu Shooting August 28 2019, ukitarajiwa kupigwa uwanja wa Taifa
Baada ya michezo ya kalenda ya CAF, Septemba 18 Yanga itasafiri mkoani Mbeya kuikabili Mbeya City katika uwanja wa Sokoine
Septemba 21 itarudi tena Sokoine kuikaili Tanzania Prisons
Oktoba 02 Yanga itarejea jijini Dar es salaam kuikabili Polisi Tanzania kisha kupisha wiki mbili za kalenda ya michezo ya CAF
Oktoba 20 itasafiri mkoani Mwanza kuikabili Alliance Fc
Kwenye mzunguuko wa kwanza Yanga itakuwa nyumbani katika michezo tisa na Ugenini michezo 10 na mzunguuko wa pili itakuwa na michezo 10 nyumbani na tisa ugenini

No comments:
Post a Comment