Na Timothy Itembe, Mara
Mkuu wa mkoa Mara, Adamu Malima jana katika kikao cha baraza cha kupitisha Hoja za mkaguzi wa halmashauri ya Rorya kwa mwaka 2017/2018 amewaasa madiwani Viti maalumu juu ya kufanya ziara kwa wananchi ndani ya maeneo husika bila kuhofu madiwani wa kata.
Malima alisema madiwani viti maalumu wanayo nafasi kuwa na mchango kwa wananchi kuwatembelea na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili hususani kutafsiri dhana ya uchaguzi Huru na haki unaozingatia Demokorasia pamoja na miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwao.
Pia Malima aliwataka madiwani kutobweteka na nafasi waliopewa badala yake wafanye kazi kama walivyoomba kwa wananchi ili kuwatumikia huku wakitatua kero mbalimbali ambazo wanauwezo nazo.
“Madiwani viti maalumu fanyeni kazi bila kukwamishwa na kama mkikwamishwa mnatakiwa kuniona fuatilia huduma za jamii,kutafsiri dhana ya uchaguzi unaozingatia demokrasia na miradi inayotekelezwa”alisema Malima.
Kwa upande wake diwani viti maalumu kupitia Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema,Mery Thomas kata ya Kitembe alisema kuwa kunachangamoto nyingi wanakuimbana nazo madiwani viti maalumu hususani madiwani wa kata kuwaona kwa jicho la kejeri.
Maye Mkurugenzi wa halmashauri ya Rorya, Charles Chacha alisema kuwa halmashauri yake ina madiwani kati ya Saba wa viti maalumu na kuwa wanaushirikianao na halmashauri.
Madiwani wangu viti maalumu hatuna shifda nao na kama wakiomba magari kwaajili ya kutembelea miradi ya wananchi iliyotekelezwa ndani ya maeneo husika halmashauri hatuna shida tunawapatia aliongeza kusema Chacha.
Chacha alimaliza kwa kusema kuwa halmashauri yake inakumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukusanyaji wa mapato jambo ambalo linasababisha miradi mbalimbali kutokamilika kwa wakati.
No comments:
Post a Comment