Chama cha Mapinduzi (CCM) kimefanya mabadiliko ndani ya Kamati Kuu ya chama hicho kwa kumwondoa Khadija Shabani Taya maarufu ‘Keisha’ baada ya kukitumikia chombo hicho nyeti kwa siku 396.
Keisha, ambaye ni msanii wa muziki wa kizazi kipya, uteuzi wake kwenye Kamati Kuu ulionekana kama angekuwa kiungo cha kuleta uhamasishaji wa sera za chama kwa wasanii nchini.
Msanii huyo ambaye ni kada wa CCM aliteuliwa kuingia kwenye chombo hicho cha uamuzi Mei 28, 2018. Kamati Kuu ina wajumbe 24 wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli.
Uamuzi wa Keisha kuondolewa ulitangazwa Ijumaa iliyopita Juni 28 katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kilichokutana Dar es Salaam na kuongozwa na mwenyekiti wake, Rais Magufuli.
No comments:
Post a Comment