Jeshi la Polisi nchini limesema kuwa wananchi ambao wamepoteza baadhi ya nyaraka zao muhimu ikiwemo line za simu, pamoja na vyeti wanaweza kupata taarifa ya utambuzi wa polisi (Loss Report) kwa njia ya kieletroniki endapo watakuwa na Kitambulisho cha Taifa.
Kauli hiyo ya Jeshi la Polisi imetolewa na Mkuu wa Mawasiliano kwa njia ya Kimtandao Gabriel Mukungu wakati akizungumza kwenye kipindi cha East Africa Breaksfast cha Eaast Africa Radio kuhusiana na mfumo mpya wa upatikanaji wa taarifa ya polisi (Loss Report) kwa njia ya kimtandao.
"Kama una kitambulisho cha Taifa, na umepoteza baadhi ya nyaraka zako kwa kutumia kitambulisho cha taifa unaweza kupata loss report, kwa njia ya kieletroniki" amesema Mukungu
"Taarifa hiyo inaweza kutolewa akiwa mahali popote pale ilimradi awe na kifaa cha kieletroniki chenye internet atakachotumia kutolea taarifa. Ili kutoa taarifa bila kufika kituoni inambidi mwananchi kutembelea tovuti ambayo nimeitaja awali ambayo ni https://lormis.tpf.go.tz inayopatikana kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza. Akishaingia kwenye tovuti atabonyeza kitufe cha “ S a jili M a li I li y o p o t e a ” na ataendelea kujaza fomu atakayoipata, baada ya kujaza fomu hiyo atatakiwa kufanya malipo."
Kuhusiana na wananchi wanaopoteza simu ambao wamekuwa hawatoi taarifa kwa Jeshi la Polisi ili kupata Loss Report Kamanda Mukungu amesema, watu hao watahesabika kama wahalifu wengine endapo line zao zitatumika kwenye uhalifu.
"Mtu akipoteza simu ya mkononi atachukuliwa na Jeshi la Polisi ili wajiridhishe kama sio wewe uliyetumia kwenye uhalifu, kwa kifupi atakuwa matatizoni wakati uchunguzi unaendelea, na kama atakuwa hakutoa taarifa polisi maanake atakuwa ni mhalifu." amesema Gabriel Mukungu
No comments:
Post a Comment