We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Thursday, June 27, 2019

Zitto Kabwe ampigia saluti Rais Magufuli, Adai yupo tayari kwa lawama ‘Najua wengi watalaumu maamuzi yangu, Ila naunga mkono serikali’

Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT Wazalendo, Mhe. Zitto Kabwe amesema kuwa licha ya yeye kuwa mpinzani lakini ataendelea kuipongeza Serikali ya Rais Magufuli.
Zitto kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika “ACT Wazalendo kimekuwa chama kinachohubiri Ujamaa lakini kwa kuingia huku kwa Maalim Seif ambaye kwenye chama chake cha CUF walikuwa wakitumia mfumo wa Kibepari inabidi tuhamie huko sasa kama tulivyokubaliana na kutakuwa na mabadiliko ya Kiuongozi.“.
Ni kweli tumekuwa tukiikosoa Serikali kwa muda mrefu lakini lazima nikiri kuwa kuna mabadiliko makubwa sana yamefanywa na Serikali hii ya JPM. Japokuwa najua kuna baadhi ya viongozi aliowateua wanamuangusha kiuhalisia MAGUFULI amefanya mengi.” ameandika Zitto Kabwe na kusisitiza.
Wapo ambao najua wataniita majina mengi ya ajabu kwa maamuzi yangu haya kama jinsi ambavyo wamekuwa wakimshambulia ndugu yangu  kwa kutokuwa na misimamo thabiti lakini nataka niwaambie huo ndio msimamo wangu na sitaki kuyumbishwa kwani hata Wanakigoma wamefaidika.” amemaliza Zitto Kabwe.
Hata hivyo, Chama cha ACT Wazalendo kimesema kuwa Tweets hizo sio za Zitto Kabwe kwani simu na laptop yake vipo mikononi mwa jeshi la polisi.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list