Beki bora nchini upande wa kulia Shomari Kapombe amesaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuwatumikia mabingwa wa Tanzania Bara Simba
Kapombe ambaye alikosa sehemu kubwa ya msimu uliopita kutokana na majeruhi, amepona majeraha hayo ambapo uongozi wa Simba umethibitisha kuwa, atakuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo kitakachokwenda kuweka kambi nje ya nchi
"Beki bora wa kulia nchini Shomari Kapombe amesaini mkataba mpya wa miaka miwili ambao utamwezesha kuendelea kuwa sehemu ya kikosi cha Mabingwa. Shomari kwa sasa yupo fiti kucheza na atakuwa sehemu kikosi ambacho kitaenda nje ya nchi kujiandaa na msimu mpya," imesema taarifa ya Simba Sc

No comments:
Post a Comment