Miongoni mwa wachezaji ambao wataendelea kubaki Simba kwa ajili ya msimu ujao ni beki Zana Coulibaly ambaye anatarajiwa kurejea wakati wowote ili kusaini mkataba mpya
Licha ya mashabiki wa Simba kuwa na maoni tofauti kuhusu beki huyo, inaelezwa kocha Patrick Aussems bado ana imani nae na ameagiza aongezwe mkataba
Hata hivyo habari njema kwa Simba ni kuwa beki wake tegemeo nafasi ya kulia Shomari Kapombe amepona majeraha na hivyo uwepo wa Zana itakuwa kumsaidia Kapombe
Uongozi wa Simba uko mbioni kukamilisha usajili ambapo huenda mwishoni mwa wiki wachezaji wote waliosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao watawekwa hadharani

No comments:
Post a Comment