Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaotumia nembo ya klabu hiyo kutengeneza jezi na vifaa mbalimbali bila kupata idhini
Aidha Yanga imetoa siku nne kwa wafanyabiashara hizo kuwasiliana na uongozi
Akizungumza na waandishi wa habari leo Makao Makuu ya klabu ya Yanga jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema baada ya Juni 30 mwaka huu wote watakaojihusisha na uuzaji wa jezi feki watachukuliwa hatua
Dk Msolla amesema Yanga iko tayari kushirikiana na watu hao na ndio maana wamewaita mezani kabla ya kuanza kuchukuliwa kwa hatua kwa wale ambao wataendelea na biashara hiyo bila kupata idhini ya klabu
Uongozi wa Yanga umejipanga kunufaika na mauzo ya jezi za klabu hiyo ambazo kwa miaka mingi wajanja wachache wamekuwa wakinufaika
No comments:
Post a Comment