We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, June 28, 2019

Amuua ndugu yake kisa kupendwa na baba

Mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Kitagutiti Kijiji cha Getenga Kata ya Mbogi Wilayani Tarime, Hassan Chacha(7), ameuawa kwa kushambuliwa na kaka yake kwa kumning'iniza juu na kumtupa chini.

Kijana aliyefanya tukio hilo, ameejulikana kwa jina la Mniko Chacha (20), ambapo chanzo chake kimetajwa kuwa ni kutokana na mdogop wake kupendwa sana na baba yao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Tarime /Rorya, Henny Mwaibambe amethibitisha tukio hilo ambapo amesema, "inasikitisha sana! kaka wa marehemu alimwambia marehemu kuwa kwanini wewe unapendwa sana, marehemu huyo ni mapacha Kurwa na Dotto, aliyefariki ni Dotto, ukiangalia umri wa watoto ni mdogo ni lazima wapendwe tu kaka yao ni mtu mzima hakupaswa kufanya huo ukatili", amesema Mwaibambe.
"Alimshambulia kwa kumning'iniza juu na kumtupa chini mara mbili akidai kwanini anapendelewa na baba yao kwa kuitwa mara kwa mara jikoni, marehemu alipata maumivu ambapo alikimbizwa katika kituo cha afya cha Dk. Steven na alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu", ameongeza.
Aidha Kamanda Mwaibambe amesema kuwa mtuhumiwa alitoroka baada ya kutenda tukio hilo na juhudi za kumtafuta na kumkamata zinaendelea.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list