We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Saturday, June 1, 2019

Watanzania 10,000 kupata ajira mradi wa Bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki


Na. Amiri kilagalila, Njombe

Wantanzania 10,000 wanatarajiwa kunufaika na ajira katika mradi mkubwa wa bomba la mafuta Ghafi la Afrika mashariki (EACOP) unaotarajia kuanza ujenzi wake mapema mwezi September mwaka huu ukiwa unapitia mikoa 8 wilaya 24 na kata 134 nchini Tanzania.

Hayo yamesemwa leo Juni mosi mwaka huu wakati wa kongamano la wadau wa Mkoa Kagera kuhusu mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki la EACOP na waziri wa nishati Mhe.Medad Kalemani kwenye hotuba yake ya ufunguzi katika ukumbi wa E.L.C.T Bukoba ambapo amewataka watanzania kuchangamkia fursa hiyo.

Amesema kuwa katika ujenzi na utekelezaji wa mradi huo kipaumbele kitatolewa kwa watanzania wa maeneo ambayo mradi huo unatarajiwa kupita kwa kuzingatia sifa na vigezo ambapo wananchi wa mkoa wa Kagera wanatarajiwa kunufaika zaidi kwasababu mradi huu unaanzia mkoani humo.

Waziri Kalemani amesema kuwa mradi huo utakuwa na kambi kubwa mbili katika mkoa wa Kagera ambazo zitakuwa katika wilaya za Missenye na Muleba ambapo amewataka wananchi wamaeneo hayo kuchangamkia fursa zote zitakazotangazwa zikiwemo fursa za kusambaza vyakula,vifaa vya ujenzi, pamoja na fani mbalimbali.

Amesema kuwa bomba hilo lenye urefu wa km 1445 urefu wa km 1147 utakuwa Tanzania sawa na asilimia 80 ambapo asilimia 20 zitakuwa nchini Uganda hivyo watanzania wameaswa kulilinda bomba hilo ili liweze kutoa huduma  kubwa ya kusafirisha mafuta huku moja ya Pump ya kusukuma mafuta itakuwa mkoani Kagera maeneo ya Kyaka wilayani Missenye.

“Katika mkoa wa Kagera kata 20 zitapitiwa na mrdi huu, vijiji 34 na vitongoji 117, kwahiyo wanankagera watakuwa na wajibu mkubwa sio kulilinda tu lakini kupata fursa nyingine. Tukumbuke ambapo bomba hili litapita miji itakuwa hivyo na ulizi utaimalika zaidi.”

Kwa upande wake, Naibu waziri wa nishati Subira Mgalu ambaye ni mlezi wa mkoa wa Kagera kwa upande wa nishati amewataka wananchi wa kagera kuchangamkia fursa hiyo na kuahidi kutoa ushirikiano ili kufikia faida za mradi  kwa wanakagera, na kuongeza kuwa vijiji vyote vitakavyopitiwa na mradi wa bomba la mafuta vitapelekewa umeme.

Mkuu wa Mkoa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti amemuhakikishia waziri wa nishati kuwa wananchi wa Kagera wapo tayari kuupokea mradi huo mkubwa na fursa zote zitakazojitokeza wanakagera watazichangamkia.

Bomba hilo la mafuta ghafi la Africa mashariki EACOP lenye urefu wa km 1445 litapita katika mikoa ya Kagera,Geita,Shinyanga,Tabora,Singida,Dodoma,Manyara na Tanga.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list