Msanii wa Muziki Bongo, Tunda Man amesema kuwa hawezi kuitungia nyimbo Timu ya Yanga hata amepewa Milioni 100.
Tunda amesema kuwa hata kama kwenye huo wimbo wagharamie kila kitu, hawezi kuiimbia timu hiyo kwasasa ataimba vibaya.
"Siwezi kuwatungia Yanga nyimbo, hata kama wimbo umelipiwa kila kitu , siwezi hata milioni 100 kwasababu ntakuwa muongo alafu mm sio mnafki, nikisema niimbe wimbo wa Yanga lazima uwe mbaya," alisema Tunda Man kwenye Mo Simba Awards.
No comments:
Post a Comment