Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kimeingia kambini leo kuanza maandalizi ya fainali za AFCON 2019 zitakazofanyika baadae mwezi huu nchini Misri
Stars imeweka kambi katika Hotel ya Whitesands iliyoko jijini Dar es salaam
Baadhi ya nyota walioingia kambini miongoni mwao ni kinda Adi Yusufu anayecheza timu ya ligi daraja la kwanza Uingereza, Blackpool
Wachezaji wote 39 walioteuliwa mwezi uliopita na kocha Emmanuel Amunike wataingia kambini ambapo wachezaji saba watachujwa
Kikosi cha wachezaji 32 kitaondoka Juni 07 kuelekea nchini Misri kufanya maandalizi ya mwisho ambapo Juni 13 kitacheza mchezo wa kirafiki na wenyeji wa michuano hiyo, Misri
Stars imepangwa kundi C pamoja na Algeria, Senegal na Kenya
Itaanza kampeni ya kuwania ubingwa wa Afrika Juni 23 kwa kuumana na Senegal
No comments:
Post a Comment