Uongozi wa Yanga unakusudia kuanzisha utaratibu wa kutambulisha kikosi chake kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya Tanzania Bara
Kwa kuanzia msimu ujao, Yanga inakusudia kutambulisha wachezaji wake kwenye baadhi ya mikoa kabla ya kuanza msimu
Lengo la utaratibu huo ni kuwapa fursa mashabiki na wachama wa Yanga kuwafahamu wachezaji wao kabla ya kuanza kwa msimu
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Omary Kaya amesema kabla ya kuanza kwa msimu mpya, zoezi hilo litafanyika kwa takribani wiki nzima kwenye mikoa mbalimbali
Zoezi hilo sio kwamba litawapa fursa mashabiki kuwafahamu wachezaji wao pekee, lakini pia litainufaisha Yanga kwa kuiongozea mapato
No comments:
Post a Comment