Akizungumza hayo jana Jumatano Juni 26, 2019 wakati wa uzinduzi wa utambulisho wa LATRA, nembo na wimbo amesema mafunzo hayo yanatolewa kwa kushirikiana na ufadhili wa Benki ya Dunia (WB).
Kamwelwe amesema mafunzo hayo yanalenga kuwaandaa na kuwajengea uwezo wakina mama hao kuendesha magari ya mwendo kasi na magari makubwa ya abiria.
Amesema hiyo ni fursa kwa akina mama ya kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa nchi hivyo kila mwenye sifa zitakazohitajika kujitokeza kushiriki mafunzo hayo.
"LATRA itawatangazia utaratibu wa kujiunga na sifa zinazotakiwa kwa muombaji, chini ya Serikali hii ya awamu ya tano hakuna kundi litakaloachwa nyuma katika kutengenezewa mazingira ya kujitafutia kipato cha kujiimarisha kiuchumi," amesema Kamwelwe.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Gilliard Ngewe amesema kuwepo kwa mamlaka hiyo ni baada ya Serikali kuigawa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) ambayo imekuwa taasisi mbili tofauti ambayo ni Udhibiti wa Shehena na Usafiri wa Majini itatekelezwa na (TASAC) na LATRA itashughulika na kudhibiti usafiri wa nchi kavu.
No comments:
Post a Comment