We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, June 28, 2019

Wachimba mgodi 36 wafunikwa na mgodi na kufariki papo hapo

Takriban watu 36 wamefariki katika mgodi mmoja siku ya Alhamisi baada ya upande mmoja wa mgodi huo wa shaba kuporomoka kusini mashariki mwa Congo, kulingana na gavana wa mkoa huo.
Ajali hiyo ilitokea katika shimo la mgodi huo wa kampuni ya Kamoto Copper Company KCC , ambayo ni kampuni tanzu ya kampuni kubwa ya uchimbaji madini duniani Glencore yenye umiliki wa asilimia 75, ya hisa zake alisema Richard Muyej Gavana wa mkoa wa Lualaba.
''Ajali hiyo ilisababishwa na wachimbaji haramu waliovamia mgodi huo'', aliambia shirika la habari la Reuters, hatua hiyo ilifanya eneo moja la mgodi huo kuporomoka katika shimo hilo.
''KOV ni eneo linaloweza kuharibika kwa urahisi na ni hatari'', aliongezera.
Kampuni ya Glencore ilisema katika taarifa kwamba imethibitisha kuwa takriban watu 19 walifariki na ilikuwa inasaidia katika kuwasaka na kuwaokoa manusura kwa ushirikiano na utawala wa eneo hilo.
Uchimbaji wa madini wa kiwango kidogo karibu na uchimbaji mkubwa wa kibishara ni tatizo kubwa barani Afrika.
Wachimbaji hao wanaotumia mbinu za kale na wasio na bima yoyote uhatarisha maisha yao.
Mikasa ya migodi nchini Congo husababisha vifo vya makumi ya watu kila mwaka.

Mgodi wa Acacia nchini Tanzania

Maelfu ya wachimbaji haramu hufanya operesheni zao kusini mwa Congo, ambayo huzalisha nusu ya idadki kuwaba ya Madini ya Cobalt duniani -yakiwa kiungo muhimu katika betri za magari ya kutumia umeme.
Glencore imesema kuwa takriban wachimbaji haramu 2000 huingia kwa siri kila siku katika mgodi huo wa KCC ambao upo karibu na mji wa Kolwezi karibu na mpaka wa Zambia na ni mojawapo wa migodi yenye madini mengi ya shaba.
Delphin Monga, katibu wa muungano wa wachimba migodi ambao unawakilisha wafanyakazi wa KCC , anasema kuwa mwanya katika eneo moja la shimo hilo ulikua umeonekana siku ya Jumatano.
Alisema kuwa KCC ilikuwa imeweka onyo kwa rangi nyekundu , lakini wachimbaji hao walikaidi.

Maafa katika migodi

Hiki sio kisa cha kwanza katika mgodi huo.
Mwaka 2016, ukuta wenye urefu wa mita 250 ndani ya KOV uliporomoka na kuwau watu saba.

Ramani ya DR Congo

Muyej amesema kuwa utawala a eneo hilo ulikuwa unaanda kikao cha kujadiliana na vipi wanaweza kuweka mikakati mipya ya kuimarisha usalama wa raia katika migodi mikubwa.
Takriban wachimba migodi tisa walifariki nchini Zimbabwe wakati waliponaswa chini ya shimo mwezi uliopita.
Wakati huohuo wachimba mgodi wqengine 22 katika mgodi mwengine wa Zimbabwe walifariki baada ya mgodi huo kukumbwa na mafuriko mnamo mwezi Februari huku wachimba migodi wengine 14 wakizikwa hai nchini Rwanda baada ya mvua mnamo mwezi Januari.
Mnamo mwezi Fenbruari watu 20 walifariki wakati gari lililokuwa likibeba tindi kali kuelekea katika mgodi wa Glencore wa Mutanda nchini DRC lilipogongana na magari mengine mawili.
Serikali ya Congo iliwapeleka wanajeshi wengi wiki iliopita kulinda mgodi wa shaba na Cobalt unaomilikiwa na kampuni ya China ya Molybdenum Co Ltd kutoka kwa wachimbaji haramu.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list