Kiungo wa Gor Mahia Francis Kahata anayetajwa kuwa mbioni kujiunga na Simba, ameshindwa kun'gara kwenye michuano ya Afcon inayoendelea nchini Misri
Kahata kiungo fundi wa kupiga pasi za mwisho, jana kwenye mchezo dhidi ya Tanzania alitolewa baada ya dakika 30
Kiungo huyo pia hakufanya vizuri kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Algeria
Kahata ameshindwa kuonyesha ubora wake, presha ya michuano hiyo mikubwa kabisa barani Afrika ikitajwa kumuharibia
Wakenya wengi kwenye mitandao ya kijamii wamemkosoa kwa kucheza chini ya kiwango ambapo wengine wamekwenda mbali zaidi wakihofia kuwa huenda thamani yake ikashuka
Timu kadhaa ikiwemo Simba zimekuwa zikiwania saini yake
No comments:
Post a Comment