Timu ya taifa ya Kenya kupitia kwa nahodha wao Victor Wanyama ameeleza siri ya ushindi wa 3-2 wa Kenya dhidi ya Tanzania katika michuano ya AFCON 2019 ni kuwa unatokana na Tanzania kupaniki na kucheza mchezo wa kupoteza muda, kitu ambacho kiliwafanya waamini kuwa hawa wana hofu na sisi kama tukiwapa presha tunaweza kuwafunga.
“Tunaweza vile tumetulia na mpira tumetengeneza nafasi nyingi tumeshinda, tulijua kidogo wao walikuwa wamepaniki maana walikuwa wanapoteza muda wanaanguka wanalala chini ni kama tulinusa hiyo kuogopa kidogo lakini tukasema hawa watu hawawezi kumaliza na sisi tukiendelea kuwasukuma kwa hivyo tunajuwa wachezaji wetu wana nguvu wanaweza kucheza hadi dakika 100”>>>Wanyama
Kenya anakuwa na nafasi kubwa ya kuwania kucheza hatua ya 16 bora bora ya AFCON 2019 kwani ana point tatu sawa na Senegal atakayecheza nae mchezo wa mwisho wa Kundi C atakachotakiwa ni kushinda ili kuwa na point sita, sare au apoteze kwa idadi ndogo ya magoli na asubiri mbeleko ya Best Looser ambayo Tanzania anaweza kuipata kwa nadra sana kama atapata ushindi na Kenya na Senegal mmoja wao afungwe magoli mengi katika mechi yao.
No comments:
Post a Comment