Licha ya kiungo Ibrahim Ajib kuhusishwa na kurejea Simba, Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema bado wanamuhitaji Ajib kwa ni mchezaji mzuri na msimu uliopita alikuwa msaada mkubwa kwa mabingwa hao wa kihistoria
Inaelezwa Ajib tayari amepokea fedha za awali za usajili kunako klabu ya Simba lakini Mwakalebela amesema wako tayari kuwapiku wapinzani wao ili kumbakisha kiungo huyo kinara wa pasi za mabao msimu uliomalizika
Mwakalebela amesema wamedhamiria kutengeneza kikosi imara kwa ajili ya msimu ujao na ndio maana wanafanya usajili wa nguvu
"Wachezaji wote tunaowasajili sasa ni mapendekezo ya kocha Mwinyi Zahera. Kuhusu Ajib ni mchezaji mzuri aliyekuwa na mchango mkubwa sana kwenye timu yetu msimu uliomalizika. Tumemwambia Yanga imenoga sasa hana sababu ya kuondoka," amesema
Aidha Mwakalebela amesema wamekusudia kumaliza zoezi la usajili mapema ili timu ipate muda wa kutosha wa kukaa kambini kabla ya kuanza msimu mpya
Amesema Yanga inatarajiwa kwenda kuweka kambi nje ya nchi ambapo hivi karibuni Zahera alifichua kuwa wanaweza kwenda kuweka kambi China
No comments:
Post a Comment