Juzi kwenye hafla ya Mo Simba Awards, Patrick Gakumba, wakala wa Meddie Kagere alikuwepo kwenye hafla hiyo baada kupewa mwaliko na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba Sc, Mohammed Dewji 'Mo'
Inaelezwa baada ya hafla, Gakumba alifanya kikao na Mo pamoja na mabosi wa Kamati ya Usajili ya Simba ambapo aliwasilisha majina ya wachezaji ambao wanaweza kusajiliwa na Simba
Wachezaji wanaotajwa kuletwa na Gakumba ni Waganda wawili, kiungo Ibrahim Sadam Juma kutoka KCCA na mshambuliaji Juma Balinya anayekipiga na Polisi ya Uganda
Mwingine ni beki Ange Baresi Gloudoeu anayekipiga klabu ya ES De Metlaoui
Gakumba ndiye aliyefanikisha usajili wa Kagere kutua Simba akitokea klabu ya Gor Mahia
Pia anamsimamia mshambuliaji mwingine wa Gor Mahia, Jacques Tuyisenge ambaye kuna wakati alikuwa akihusishwa kusajiliwa na Simba
"Nimekuja hapa Tanzania baada ya kualikwa na Mo kwenye hafla ya tuzo za Simba. Tumeongea mambo mengi, mengine mtayasikia kutoka kwa viongozi wa Simba," Gakumba aliwaambia waandishi wa habari
"Simba ni timu kubwa yenye mipango mizuri, nadhani wanaweza kutwaa ubingwa wa Afrika siku moja"
Kuhusu mchezaji wake Kagere, Gakumba amethibitisha kuwa ana ofa tatu, mbili zikitoka klabu za Zamaleki na Mamelodi Sundowns
Hata hivyo Gakumba amesema Kagere bado ni mchezaji wa Simba, maamuzi ya mwisho yatatolewa na viongozi wa timu hiyo
No comments:
Post a Comment