Mlinzi wa kati Ange Baresi Gloudouei ni miongoni mwa wachezaji watatu walioletwa na Wakala Patrick Gakumba ili waweze kusajiliwa na Simba
Gloudouei mwenye umri wa miaka 32 anatokea klabu ya ES METLAOUI na ameletwa kuchukua nafasi ya Juuko Murshid ambaye mkataba wake umemalizika
Beki huyo mrefu ana uzoefu wa soka la Afrika kwani amewahi kuzichezea Horoya Athletic ya Guinea na Asec Mimosas ya Ivory Coast
Wachezaji wengine wlioletwa na Gakumba ni Waganda wawili, kiungo Ibrahim Sadam Juma kutoka KCCA na mshambuliaji Juma Balinya anayekipiga timu ya Polisi ya Uganda
No comments:
Post a Comment