We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Sunday, June 2, 2019

NIYONZIMA AVUNJA UKIMYA SIMBA SC

KIUNGo machachari wa simba, Mnyarwanda Haruna Niyonzima, amevunja ukimya kuwa mpaka sasa uongozi wa timu hiyo haujazungumza naye ishu yoyote ya kuongeza mkataba na kwamba hilo halimtishi kwani ana ofa kibao.

Niyonzima alijiunga na Simba misimu miwili iliyopita akitokea Yanga, alianza kazi Msimbazi kwa kusuasua kutokana na majeraha kabla ya kuibuka hivi karibuni na kuonyesha kiwango kizuri.

Kwa sasa mkataba wake Msimbazi umemalizika. Akizungumza na Championi Jumamosi, Niyonzima alisema, anapenda kuendelea kucheza Simba licha ya kuwa mkataba wake umekwisha na hajaambiwa lolote na viongozi wa timu hiyo.

Alisema hata kama Simba hawatampa mkataba mwingine haina shida kwani ana ofa nyingi ambazo amezipata. “Mimi ningependa sana kuwepo Simba lakini kwa sasa napata kigugumizi kusema lolote kwa kuwa mkataba umeisha na sijaambiwa lolote na uongozi.

“Watu wajue kuwa hapa (Tanzania) pameshakuwa kama nyumbani na nisingependa kuondoka, lakini itategemea uongozi unasemaje maana mwisho wa siku namaliza mkataba kwa hiyo siwezi kung’ang’ania kama wao hawanihitaji,” alisema Niyonzima.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list