Timu za Kagera Sugar na Mwadui Fc leo zitashuka viwanjani ugenini kutetea nafasi zao za kubaki ligi kuu dhidi ya timu za daraja la kwanza Pamba Fc na Geita Gold
Kagera Sugar ambayo awali ilikumbana na 'janga' la kushushwa daraja na Bodi ya Ligi kutokana na uzembe uliofanywa na Bodi hiyo kwa kutokuwa na takwimu sahihi, itaanzia ugenini uwanja wa Nyamagana kuumana na Pamba Fc 'Wana Kawekamo'
Wakati Mwadui Fc itakuwa ugenini kuumana na Geita Gold
Michezo yote itapigwa saa kumi jioni na itarushwa mbashara na Azam Tv
Michezo ya marudiano itapigwa wiki ijayo, Juni 08, Kagera Sugar itakuwa nyumbani dimba la Kaitaba na Mwadui Fc itakuwa nyumbani uwanja wa CCM Kambarage
Timu zitakaibuka na ushindi wa jumla baada ya michezo yote miwili, zitacheza ligi kuu msimu ujao wakati nyingine mbili zitacheza ligi daraja la kwanza
No comments:
Post a Comment