Barcelona inataka kumsaini mshambuliaji wa Atletico Madrid na Ufaransa Antoine Griezmann, 28, na mshambuliaji wa PSG na Brazil Neymar, 27. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Juventus inajiandaa kulipa fidia ili kumnunua mkufunzi Maurizio Sarri kutoka Chelksea. . (Independent)
Beki wa Napoli mwenye umri wa miaka 25 na raia wa Albania Elseid Hysaj amethibitisha kwamba ana lengo la kuondoka katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu, akiongezea kwamba anataka kushinda chochote katika mchezo wake . Ananyatiwa na klabu za Chelsea na Manchester United. (DigitAlb via Talksport)
Chelsea itajaribu kumsaini kiungo wa kati wa Brazil na Barcelona Philippe Coutinho, 26, iwapo watabadilisha marufuku yao ya kutosajili wachezaji. (Gianluca di Marzio)
Mkufunzi wa Leicester City Brendan Rodgers atajaribu hamu ya klabu ya Crystal Palace kumuhifadhi winga wa Uingereza mwenye umri wa miaka 27 Andros Townsend. (Mirror)
Newcastle United haijazungumza na kocha wa zamani wa AC Milan Gennaro Gattuso kama mkufunzi atakayerithi mahala pake mkufunzi wa sasa Rafael Benitez. (Newcastle Chronicle)
Mwenyekiti wa Liverpool Tom Werner amesema kuwa kampuni ya michezo ya Fenway Sports Group haina nia ya kuiuza klabu hiyo iilioshinda kombe la mabingwa Ulaya. (Liverpool Echo)
Arsenal itataka kumsaini beki wa kulia wa PSG mwenye umri wa miaka 27 Thomas Meunier. (Paris United)
Klabu ya Fiorentina, ambayo iliepuka kushushwa daraja kutoka ligi ya Serie A katika wikendi ya mwisho ya mechi inauzwa. (Corriere della Sera - in Italian)
Mchezo wa kiungo wa kati wa Sporting Lisbon anayenyatiwa na Manchester United Bruno Fernandes, 24, umemshangaza aliyekuwa mkufunzi wa man United Jose Mourinho. (Mirror)
Wakati huohuo mshambuliaji wa barcelona amesema kuwa ana kundi la WhatsApp la kibinafsi na neymar na mchezaji mwenza Luis Suarez.
Inter Milan ina hamu beki wa Roma Aleksandar Kolarov, 33. (Gazzetta dello Sport - in Italian)
No comments:
Post a Comment