Baada ya Ligi Kuu Tanzania bara kumalizika na Simba kushinda ubingwa huo, ni wakati sasa wa klabu mbalimbali kufanya usajili kwa ajili ya msimu ujao.
Tetesi zinazosambaa hivi sasa zinawahusisha wachezaji, Francis Kahata wa Gor Mahia na Ally Ally wa KMC.
Inaelezwa kuwa Ally Ally yuko katika mazungumzo mazuri na klabu ya Yanga, ambapo muda wowote anaweza kumwaga wino katika klabu hiyo ambayo ipo katika mkakati mzito wa kusuka kikosi chake kuelekea msimu ujao.
Francis Kahata naye kwa mujibu wa chanzo chetu, yuko katika mazungumzo makubwa na mabingwa wa soka nchini, Simba na kuna uwezekano wa asilimia 75 za kutua katika klabu hiyo.
Makubaliano ya Kahata na Simba yanaweza kumalizwa kabla au baada ya kumalizika kwa michuano ya AFCON inayotarajia kuanza Juni 21 nchini Misri.
Tayari tetesi zingine za kusajili wachezaji mbalimbali zinaendelea kwa upande wa Yanga huku nyota kadhaa wa ndani na kimataifa wakitajwa kumalizana na klabu hiyo. Kati ya hao yupo beki Lamine Moro kutoka Buildcon FC ya Zambia pamoja na Papy Sibomana kutoka Mukura Victory ya Rwanda.
Wengine ni Abdulaziz Makame kutoka Mafunzo ya Zanzibar na Issa Bigirimana kutoka Armée Patriotique Rwandaise ya Rwanda. Wachezaji wengine ni Ally Mtoni Sonso kutoka Lipuli FC na Mohamed Ally Camara kutoka Guinea.
No comments:
Post a Comment