Mshambuliaji wa klabu ya PSG, Neymar Jr amekumbwa na tuhuma za ubakaji nchini Ufaransa.
Taarifa kutoka katika duru za habari nchini Ufaransa, zinaeleza kuwa Neymar alimsafirisha binti huyo wa miaka 17 kutoka Brazil mnamo tarehe 15-17 mwezi Mei mwaka huu.
Imeelezwa kuwa Neymar alimpokea binti huyo na kumpeleka katika hoteli ya Sofitel Paris Arc Du Triomphe na kutekeleza maovu hayo.
Kwa mujibu wa gazeti la El Mundo limeeleza kuwa Binti huyo na Neymar walilewa pombe usiku wa Mei 16 na waliingia hotelini hapo pasipokujua kama wanarekodiwa.
Akielezea tukio hilo mbele ya Polisi mjini Sao Paulo Brazil, Binti huyo amesema alitongozwa na Neymar kupitia mtandao wa Instagram na baadae alitumiwa tiketi ya ndege akitaka wakutane Paris Ufaransa.
Amesema alipofika Ufaransa Neymar alimfikisha kwenye hoteli hiyo na kumlazimisha kufanya mapenzi kinyume na matakwa yake.
Tayari familia ya binti huyo imefungua kesi dhidi ya Neymar.
Kwa upande mwingine, baba yake na Neymar ambaye ndiye wakala wake, amesema malalamiko hayo hayana ukweli hivyo yupo tayari kwenda mahakamani kujibu tuhuma hizo.
No comments:
Post a Comment