Vero Ignatus,Kilimanjaro.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imeendesha zoezi la kusajili laini za simu kwa mfumo wa alama za vidole ikishirikiana na Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) Jeshi la Polisi Kitengo cha makosa ya mtandaoni,Uhamiaji pamoja na watoa huduma za mawasiliano, stendi kuu ya mabasi mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Mabel Masasi ni Afisa mwandamizi wa habari na mahusiano kutoka TCRA ambapo amesema kuwa Zoezi hilo limeenda sambamba na utoaji wa elimu juu ya matumizisahihi ya vifaa vya mawasiliano,ambapo NIDA wanawasaidia wananchi kupata vitambulisho vya Taifa ambapo mzunguko huo umekuwa ukifanyika nchi nzima ambapo Kilimanjaro ni mkoawa 10.
Amesema kuwa wataendelea kuzunguka mikoa yote lengo kuu likiwa ni kufanya uhamasishaji wa kusajili kwa namba za vitambulisho vya Taifa na kwa alama za vidole na ili kurahisisha huduma kwa wananchi ambao wamejitokeza katika zoezi hilo.
Masasi amesema kuwa zipo changamoto malimbali walizokutana nazo na wamejaribu kuyatatua kadiri wanavyozidi kwenda mikoani,amesema kubwa zaidi ni vile amabavyo wananchi wengi wamekuwa wakilalamika hawazijui namba zao za vitambulksho ambapo tumewasihi NIDA waweze kutatua changamoto hiyo kwa wananchi.
Calistus Mhode ni Mkaguzi maidizi kutoka Jeshi la Polisi kitengo cha makosa ya mtandaoni amesema amesema zoezi hilo linaendelea nchi nzima la mnada kwa mnada ambapo wanashirikiana na Taasisi nyingine za serikali katika kuielimisha jamii na kuwafikia wananchi juu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii,na matumizi ya teknolojia kwa ujumla .
"Tunawataka wananchi wote wanaokuwa na changamoto zakipolisi sisi tupo tayari kuwaelimisha na kutafuta suluhu za changamoto mbalimbali amabazo zimewakumba "alisema Calistus.
Abubakari Kakinga Afisa wa NIDA mkoa wa kilimanjaro amesema kuwa wataendelea kutoa hudumakwa wananchi na kama vitambulisho vitakuwa vimechelewa wananchi wanawezakutumia namba za vitambulisho vyao kupata huduma malimbali kama usaajili wa simu zao.
Amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi na kwa wakati kujisajili ya kupata kitambulisho cha Taifa wasisubirie hadi pale zoezi litakapofungwa.
No comments:
Post a Comment