Licha ya kutofikia makubaliano mwanzo, klabu ya TP Mazembe imetuma mawakala wake kumshawishi aliyekuwa nahodha wa Yanga Ibrahim Ajib ili ajiunge na timu hiyo
Taarifa za uhakika zimebainisha kuwa Mawakala wa Mazembe bado wako nchini walikokuja kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Mbeya City Eliud Ambokile
Awali Mazembe ilikuwa ikihusishwa kumuwania beki Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' kabla ya Simba kumuongezea mkataba nahodha huyo msaidizi
Hata hivyo jitihada zao kwa Ajib nazo zitaishia ukingoni kwani tayari fundi huyo wa mpira amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba, klabu iliyomlea
Simba inaweza kumtambulisha rasmi Ajib siku ya Jumatatu, Julai 01
No comments:
Post a Comment