We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, June 28, 2019

AC MILAN YAFUNGIWA KUSHIRIKI MICHUANO YA ULAYA

KLABU ya soka ya AC Milan ya Italia yenye makazi yake katika uwanja wa San Siro, itatumikia kifungo cha mwaka mmoja kutokushiriki michuano ya Ulaya inayoandaliwa na shirikisho la soka la Ulaya (UEFA) ikiwa ni Klabu Bingwa Ulaya na Europa Ligi

Klabu hiyo iliyomaliza katika nafasi ya tano kwenye ligi ya soka Italia, Serie A,  imekumbana na kifungo kutoka kwa Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo baada ya kuvunja sheria ya ‘Financial Fair Play’ na hivyo haitashiriki michuano ya Europa ya msimu ujao

Kuna uwezekana mkubwa kuwa kwa sasa nafasi yao ya kushiriki Ligi ya Europa itachukuliwa na Torino, iliyomaliza katika nafasi ya saba kwenye Ligi ya Serie A msimu uliopita. Roma iliyokuwa nafasi ya sita  ilishafuzu.

Milan ilifanikiwa kukata rufaa dhidi ya kifungo cha miaka miwili ilichopewa awali na UEFA msimu wa majira ya joto uliopita baada ya kupatikana na hatia ya kuvunja sheria  hiyo ya ‘Financial Fair Play’

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list