Mchungaji Mashimo ameomba apelekwe nchini Misri kwaajili ya kwenda kutoa unabii aliooteshwa na Mungu ili Taifa Stars ishinde.
Mashimo amesema kuwa, wachezaji wa timu ya Taifa wako imara na wanacheza mpira vizuri, hivyo amewataka watanzania kuwa wazalendo kwa kuiombea na kwamba kuombea mpira sio dhambi.
''Kwahiyo mimi Mungu amenipa ujumbe, inayocheza kule ni Taifa Stars na mimi ni mchungaji wa taifa, nina imani kweli ya timu kuchukuwa kombe. Ebu nipeni nafasi ya kunipeleka Misri hata siku moja na kurudi ili nikatimize neno la Mungu'', amesema.
Aidha amempongeza Rais Magufuli kwakuwa na imani na Stars, kama imani aliyokuwa nayo yeye na kusisitiza afanyiwe utaratibu wa kupelekwa.
Taifa Stars ambayo tayari imeshaaga michuano hiyo huku ikisubiri mchezo wa kukamilisha ratiba, itacheza na Algeria Jumatatu Julai 1, 2019.
No comments:
Post a Comment